Naibu Waziri na Waziri wa Nishati Mhe.Doto Mashaka Biteko amesema Sekta ya nishati itaendelea kutatua changamoto zote zinazoikabili sekta hii ikiwa ni pamoja na kuhamasisha nishati safi ya kupikia pamoja na kuhakikisha asilimia 80% ya watanzania wanatumia nishati safi ya kupikia ifikapo 2030.
Biteko ameyasema hayo leo novemba 5 jijini Dodoma wakati akizungumza na wadau wa nishati na madini katika Jukwaa la uziduaji 2024 Agenda iliyoandaliwa na Haki Rasilimali.
Aidha ametoa Rai kwa wadau wa mkutano huo kwamba mijadala yote itakayokuwa inajadiliwa iwe yenye tija lakini pia majadiliano hayo Serikali itayachukua na kuyafanyia kazi ikiwa ni pamoja na kuambiana ukweli kuhusu umuhimu wa nishati safi ili kuhakikisha tunapata maendeleo Kwa pamoja kama nchi.
Kwa upande wake Waziri wa Madini Antony Mavunde amesema Sekta ya madini imeendelea kukua Kila siku kwani moja kati ya mkakati mkubwa ni kufanya utafiti wa kina katika eneo kubwa la asilimia 16 kwani nchi imepata manufaa ambapo Sekta ya madini imeingiza Dola za kimarekani bilioni 3.1 ambayo ni sawa na asilimia 56%.
Aidha ameongeza kuwa mwaka huu wa fedha wamejipanga kuingizia Serikali trilioni 1 maduhuli ifikapo mwezi wa 6 mwakani kwani nchi ya Tanzania ina madini ya kutosha na madini mkakati ambapo hivi sasa wanamkakati maalum wa kuyavuna madini mkakati.
Akitoa salam za Mkoa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule amewashukuru haki Rasilimali Kwa kuchagua mkoa wa Dodoma kuweza kufanya mkutano wao kwani wamechagua sehemu sahihi na sehemu salama.
Aidha amempongeza Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan Kwa kazi kubwa anayoifanya kwenye sekta ya madini hasa kutoa upendeleo kwa mkoa huu kwani utafiti uliofanyika unaonyesha mkoa wa Dodoma unaongoza kwa kuwa na madini mengi tofauti na mikoa mingine.
"Jengo la Makao Makuu ya Mahakama ya Tanzania nalo ni kivutio,kwani nchini, Afrika Mashariki na Afrika kwa ujumla hakuna la namna hiyo zaidi ya Dodoma"Ameongeza Senyamule
Naye Adam Anthony Mkurugenzi Haki Rasilimali amesema anawashukuru wadau pekee na washiriki kutoka Kenya,Uganda na Jamuhuri ya kidemokrasia ya Congo Kwa kukubali kuja kubadilishana uzoefu.
Aidha amesema jukwaa la uzinduaji limewakutanisha washiriki takribani 200 kutoka sehemu mbalimbali kuweza kujadili mambo mbalimbali ikiwemo ushiriki wa wanawake kwenye sekta ya madini na sekta ya nishati ikiwa ni sambamba na Serikali kukemea vitendo vya Rushwa.
Sanjari na hayo Mwenyekiti wa Bodi Haki Rasilimali Jimmy Luhende ameiomba Serikali kwa kushirikiana na wadau wengine kuangalia namna bora na Salama kimazingira Kwa wanaotumia zebaki,ikiwa ni pamoja na kutafuta namna mbadala ya kunasa madini bila kupata madhara yoyote.
"Serikali ijaribu kuwaangalia akina mama watenge maeneo ya leseni waweze kuwapatia vikundi vya kina mama kwani wanatumia nguvu kubwa kipato kidogo mfano kuponda mawe na kusafisha madini, hivyo Serikali iangalie namna bora ya kuwafikia kina mama ili waweze kujikwamua kiuchumi"Amesema Mchimbaji mdogo wa madini Ndugu.Amos Juma.
TAASISI ZA UMMA ZAHIMIZWA KUTENGA ASILIMIA 30 YA BAJETI YA MANUNUZI KWA AJILI YA WANAWAKE NA MAKUNDI MAALUM.
NIC YAZINDUA KAMPENI YA NIC KITAA ILI KUTOA ELIMU YA BIMA KWA WANANCHI.
DCEA YABAINI WAFANYABIASHARA WA SHISHA WANAOCHANGANYA BIDHAA HIYO NA DAWA ZA KULEVYA.
TUKIFANYA KAZI KWA PAMOJA TUTAPATA WATALII WA KUTOSHA UKANDA WA KARIBE NA MAENEO JIRANI - BALOZI POLEPOLE
DIAMOND ASIFIA UWEKEZAJI WA VIDEO YA "OLOLUFEMI"
MABADILIKO YA TABIA YA NCHI CHANZO CHA KUPUNGUZA UZALISHAJI WA MAZAO
TAASISI ZA UMMA ZAHIMIZWA KUTENGA ASILIMIA 30 YA BAJETI YA MANUNUZI KWA AJILI YA WANAWAKE NA MAKUNDI MAALUM.
TRENI YA MCHONGOKO KUSIMAMA KWA SAA SITA NI HUJUMA:TRC
RAIS DKT.SAMIA ANATARAJIWA KUWA MGENI RASMI KUZINDUA RASMI MFUKO WA MKOPO KWA AJILI YA KUSAIDIA BUNIFU.
AWESO,BASHUNGWA WAJADILI MIKAKATI KUTATUA CHANGAMOTO YA MAJI KATIKA JIJI LA TANGA.